26 Apr 2016

LEO WATANZANIA WOTE TUNASHEREKEA MIAKA 52 YA MUUNGANO WETU,HII NDIO HISTORIA YA MUUNGANO HUU ULIODUMU KWA MUDA MREFU NA KUDUMISHA AMANI .


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa
mnamo tarehe 26 Aprili, 1964 kwa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa
vya Pemba na Unguja). Tanganyika ilikuwa ni
mwendelezo wakoloni la Ujerumani, utawala wa
Waingereza kwa Mamlaka ya Umoja wa Mataifa,
Himaya ya Umoja wa Mataifa chini ya utawala
wa Uingereza na mwisho Taifa huru kuanzia
mwaka 1961 ndani ya nchi za Jumuiya ya
Madola.
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar ziliingia mkataba wa Muungano mnamo
mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Mkataba huu wa
Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa
Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na
aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid
Amani Karume tarehe 22 Aprili 1964 huko
Zanzibar. Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la
Tanganyika na Baraza la Mapinduzi hapo tarehe
26 Aprili, 1964 na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964,
viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika
ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es
Salaam na kubadilishana Hati za Muungano.
Sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya
Muungano katika Ibara ya 4 kwamba:
“Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku
zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa
Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya
4 Sheria za Muungano)”
Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar” lilibadilishwa baadae mnamo tarehe
28 Oktoba, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya
Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni