4 Apr 2016

HAPA NDIPO WALIPONYONGWA NA KUZIKWA MASHUJAA 66 WA VITA YA MAJIMAJI



February 27 ,1906 ni siku ambayo mashujaa 66 wa vita vya majimaji walinyongwa mpaka kufa na wajerumani huko Songea mjini.Mashujaa hawa 66 walinyongwa na kuzikwa bila sanda ndani ya kaburi moja kubwa.
Kila tarehe 27 ya mwezi wa pili Tanzania nzima hufanya sherehe za kuwakumbuka mashujaa hawa zikiambatana na kwenda kutazama na kuyafanyia usafi kwa pamoja makaburi haya.
Sehemu hiyo waliyonyongwa mashujaa hawa imekarabatiwa na kutengenezwa vizuri ikiwa  ni maalumukwa ajili ya makumbusho ya mashujaa hawa.
picha ikionesha majina ya mashujaa hawa66
Mashujaa hawa walifanyiwa vitendo mbalimbali vya kudhalilishwa wakati wananyongwa ,moja ya matukio hayo ilikuwa ni walilazimishwa kuvuta Ugoro kabla ya kunyongwa na wengine waliambiwa wabatizwe ndio wanyongwe.
Picha ikionesha kaburi moja walilozikiwa mashujaa hawa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni