8 Apr 2016

MFAHAMU 'NUNGUNUNGU' MOJA YA WANYAMA ADIMU SANA WANAOPATIKANA TANZANIA NA NCHI ZINGINE CHACHE DUNIANI.

Nungnungu ni wanyama wagugunaji wenye ngozi yenye miiba iliyochongoka wanayotumia kujilinda na maadui. Walienea katika ulimwengu wa sasa na ulimwengu wa zamani. Katika wanyama wagugunaji ni watatu kwa ukubwa, wakitanguliwa na capybara na buku. Nungu wana urefu kati ya sm 20 - 25. Uzito wao wakaribia kg 5.4 - 16. Wana umbo la duara, wakubwa na wataratibu kweli.



Nungunungu ni wanyama ambao huwa na rangi mbalimbali zikiwemo kijivu,nyeusi,kahawia ambayo imepauka kwa sababu ya rangi zake na kumfanya kuwa miongoni mwa vivutio vya utalii

Nungu wa dunia ya leo wanaumbo dogo (japokuwa nungunungu wa Amerika ya Kaskazini wanafikia kama sm 85 kwa maelfu na uzito wa kilogramu 18), 

Ni vigumu sana kuweza kuwaona kwa vile wanaishi kwa mashaka sana,maana mara tu wanapoonekana machoni pa watu hushambuliwa na kuwaua kwa sababu mbalimbali.Wengine huwaua kwa sababu ya kuwatuhumu kuwa wanakula mazao yao mashambani.Lakini wengine huwaua kwa sababu wanadai kuwa miiba yake ni dawa.

Nungunungu hupenda kuishi na kufurahia mazingira yenye mapori na misitu ili kujihadhali na ukatilii anaotendewa.Nivigumu sana kumpata mnyama kama Nungunungu katika sehemu zenye nyasi fupi fupi huwa huishi kwe sehemu zenye nyasi ndefu kwa ajili ya usalama wao.

Nungunungu hula chakula ambacho mara nyingi hulimwa na kuandaliwa na binadamu huko mwituni,ambako ndio sehemu sahihi ya maakazi ya Nungunungu.Kutokana na kuharibiwa makazi yao Nungunungu hulazimika kula mazao yaliyolimwa kama mahindi,ndizi,mihogo,na mazao mengine yanayoliwa na binadamu hiyo upelekea kuwa na uadui mkubwa na binadamu na Nungunungu kuona kuwa mazingira alimo binadamu si maeneo sahihi kwa kuishi ns kuendeleza maisha yake yote.Kwa hiyo uhama na kwenda sehemu jingine.

Nungu hupatikana sana katika maeneo ya kawaida na tropiki ya Asia, Italia, Afrika na Amerika ya Kusini na Kaskazini. Nungu huishi kwenye misitu, jangwani sehemu zenye miamba, vilima na nyikani. Baadhi ya nungu wa Dunia Mpya huishi kwenye miti, lakini nungu wa Dunia wa Kale wanakaa ardhini. Nungu huweza kupatikana hata kwenye miamba kwenye ardhi yenye hata urefu wa mita 3700. Nungunungu ni wanyama wa usiku.

Nungunungu hawazaliani kwa wingi sana kama wanyama wengine wanaoishi mwituni hii ni kwa sababu ni wanyama ambao jamii huwatumia sana kwa ajili ya kitoweo pamoja na shughuli nyingine kama dawa ya asili.

Katika Tanzania inasemekana Nungunungu huwapatikana kwa wingi katika mapori mbalimbali likiwemo pori la Nyamunsi lililoko Wilayani Tarime Mkoa wa Mara.Baadhi ya Wenyeji wa sehemu hiyo wanaamini kuwa ngozi ya Nungunungu ni dawa ya watoto wadogo na hivyo waganga wengi huwawinda na kuwatumia kwa lengo la kutibu watu kutokana na imani tofauti katia jamii.Pia Nungunungu anahusishwa sana na uchawi kwani anaaminika kuwa ukimkuta njiani ni ishara ya kutokea kwa jambo fulani baya au zuri.

Nijukumu la sisi Watanzania kuhifadhi makazi ya wanyamapori kwa kuwa ni suala la sisi sote.Wanyamapori hawa ni urithi wetu,kila mmoja wetu atimize wajibu wake kwa nafasi yake ili kuhakikisha uwo wa rasilimali ya wanyamapori na matumizi yake vinakuwa enendelevu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni