2 Apr 2016

IFAHAMU HIFADHI HII YA CHURA ANAEZAA ,CHURA HUYU ANAPATIKANA TANZANIA TU NA SIO SEHEMU NYINGINE YOYOTE HAPA DUNIANI.

Kama ilivyo kawaida kwa chura wengine wote duniani kuweza kujipatia uzazi kupitia kutaga mayai.Hali hii imekua tofauti kabisa kwa aina hii ya chura wanaopatikana katika maporomoko ya maji yaitwayo mahala yanayopatikana ndani ya milima ya Udzungwa wilayani Kilombero Mkoani Morogoro, kwani chura hawa ujipatia uzazi kupitia njia ya kuzaa kitu ambacho ni tofauti kabisa na chura wengine wote ulimwenguni.Chura huyu aligunduliwa mwaka 1996 katika maporomoko ya  milima hiyo ya Udzungwa .Utafiti ulionesha chura huyu anaishi katika mazingira ya maji yanayotiririka na kutoka kwenye mvuke wa kutosha unaotokana na nguvu za maji.


Pichani ni Bomba zilizowekwa na kutoa maji ya mvuke 'Sprinkers' kule kwenye korongo la Kihansi ambako ni makazi asilia ya chura kuwavutia chura kuishi kumejengwa na daraja la mbao kwa ajili ya kuvuka mto.
Kwa jina la kiingereza chura huyu anaitwa Spray Toad na kwa jina la kitaalamu anaitwa Nectophynoides asperiginis .
Chura huyu hutaga mayai na kuyabakiza mwilini mwake adi muda wa kuyatotoa unapowadia ndipo utotoa ndani ya mwili wake na kutoka viumbe hai vilivyototolewa bila ya mayai kutoka au kuonekana.Kwa Kifupi chura huyu tunasema anazaa sababu mayai yake huwa hayaonekani ,huonekana watoto tu waliokwisha totolewa .
Haina hii ya kuzaa ndio kitu kinachozidi kuwafanya chura hawa wazidi kuonekana ni wa pekee siku baada ya siku.
Chura huyu ni hadhina kubwa sana ya utalii hapa nchini Tanzania kwani hapatikani sehemu nyingine yoyote hapa duniani zaidi ya Tanzania kwenye milima ya Udzungwa.


Maoni 3 :

  1. asante kwa kutujuza,binafsi ninaomba kupatiwa tabia na maisha kwa ujumla kuhusu chura huyu.

    yesadeon1@gmail.com

    JibuFuta
  2. Elimu hii endeleen kutoa Elimu

    JibuFuta
  3. Naomba jina la uyu chura kwa kiswahili

    JibuFuta