3 Apr 2016
HAYA NDIO MAAJABU YA JIWE LA 'MBUJI' LINALOPATIKANA WILAYANI MBINGA MKOANI RUVUMA.
Maana ha neno 'MBUJI' ni kitu kikubwa sana.
Jiwe hili ndio jiwe kubwa kuliko yote ndani ya mkoa wa Ruvuma,ni jiwe lenye vyanzo vingi sana vya maji.
Uruhusiwi kulipanda jiwe hilo bila idhini kutoka kwa watu maalumu wanaolielewa vizuiri hilo jiwe kwani kuna mtalii mzungu alikuja kutalii kwenye hili jiwe na akajalibu kulipanda ,alikutwa ameshaaga dunia.
Jiwe hili la Mbuji ni ngumu sana na auwezi kulizunguka kwani ukianza kuzunguka na kuweka harama sehemu unapoanzia kuzunguka ukirudi hauikuti io alama.
Jiwe hili hutumika pia kwa matambiko na baadhi ya koo za eneo hilo.
Ni kivutio kikubwa sana kwa watalii wanaopenda kuwa mkoani Ruvuma.
Ni jiwe linaloheshimika sana na wakazi wa eneo hilo/
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni