26 Apr 2016

HILI NDIO DARAJA LA KIGAMBONI,DARAJA REFU AFRIKA MASHARIKI LILILOPEWA JINA LA BABA WA TAIFA.



Mnamo April 19 ya mwezi huu daraja la kigamboni lilizinduliwa rasmi na kuanza kutumika kama ilivyopangwa.Mgeni rasmi katika shughuli izo za uzinduzi wa daraja hili alikuwa mheshimiwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu John Pombe Magufuli.
Daraja hili la kisasa linalotajwa kuwa ndio daraja refu kuliko yote Afrika mashariki lina urefu wa mita 680 na upana wa mita 27.5.Daraja hili lina barabara sita za magari na barabara moja ya waenda kwa miguu kila upande.
Daraja hili limepewa jina la baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere licha ya watanzania wengi kupendekeza jina la raisi wa sasa mheshimiwa John Pombe Magufuli Lakini mheshimiwa raisi ye mwenyewe akapendekeza jina la mwalimu Nyerere litumike kama jina la daraja hilo.
Asilimia 60 ya ujenzi wa daraja hili imedhaminiwa na mfuko wa hifadhi ya taifa NSSF na asipimia 40 imetolewa na serikali ya jamhuri ya muungano wa  Tanzania.Daraja hili adi kukamilika limegharimu zaidi ya dola za kimarekani 140.





Muonekano wa daraja hill wakari wa usiku.

Maoni 1 :

  1. New slot machines in Las Vegas - JetBlue Casino Hotel
    LAS VEGAS (KTNV) -- The city is on the 이천 출장샵 edge of a 오산 출장샵 new casino-hotel project called JetBlue Vegas. It has been in 충청남도 출장샵 the 파주 출장마사지 planning 충주 출장샵 phase since

    JibuFuta