1 Mei 2016

MFAHAMU 'MOHAMMED IQBAL' MTU ALIEBUNI NENO 'TANZANIA' MPAKA KUTUMIKA KAMA JINA LA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

Huyu bwana aliyebuni jina la Tanzania ni
Muhindi na dini yake ni AHMADIYA MUSLIM. Majina yake
ni MOHAMMED IQBAL DAR.
Mohammed alizaliwa Mkoani Tanga miaka
ya 1944,Baba mzazi wa Mohammed
alikuwa Daktari huko mkoani Morogoro
alikuwa anaitwa Dr. T A DAR alikuwa
Tanganyika kuanzia mwaka 1930.
Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake
ya Msingi Mkoani Morogoro shule ya
Msingi H H D AGAKAN kwa sasa ni Shule
ya Serikali na baada ya Hapo alikuja
baadae kujiunga na Chuo cha Mzumbe
akasoma Kidato cha Kwanza mpaka cha
Sita.
Aliingiaje kwenye shindano la
kupendekeza jina la Muungano kati
Tanganyika na Zanzibar,Mohammed
anasema alikuwa Maktaba akijisoma
gazeti la Tanganyika Standard siku hizi
Daily News akaona Tangazo linasema
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
unafahamika kama Republic of
Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana
refu sana kwa hiyo Wananchi wote
wakaombwa Washiriki kwenye shindano la
Kupendekeza jina moja litakalo zitaja nchi
zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar
Mohammed Iqbal Dar anasema aliamua
kuingia kwenye Shindano na hivi ndivyo
alianza Safari ya Kubuni Jina la
Muungano,Kwanza anasema alichukua
karatasi akaandika Bismillah Raahman
Rahimu hii ni kutokana na Imani yake na
baada ya hapo akaandika jina la
Tanganyika baada ya hapo akaandika
Zanzibar halafu akaandika jina lake Iqbal
halafu akaandika jina la Jumuiya yake ya
Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena
Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili
apate jina zuri kutoka katika majina hayo
aliyokuwa ameyaandika.
Baada ya hapo Mohammed Iqbal Dar
alichukua herufi tatu kutoka Tanganyika
yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar
akachukua Herufi tatu za Mwanzo ZAN
ukiunganisha unapata TANZAN alivyoona
hivyo akachukua I herufi ya kwanza katika
jina lake la Iqbal na akachukua A kutoka
jina la dini yake yaani Ahmadiyya kwa
maana hiyo ukiongeza herufi hizi mbili I na
A kwenye TANZAN unapata jina kamili
TANZANIA akalisoma jina akaliona ni zuri
lakini akajiridhisha pia kwamba akiongeza
herufi hizo za I na A kwenye TANZAN
italeta maana kwakuwa nchi nyingi za
Afrika zinaishia na IA.
mfano
EthiopIA, ZambIA,NigerIA,TunisIA,SomalIA,GambIA,NamibIA,LiberIA,MauritanIA
alivyoona hivyo akaamua apendekeze
kuwa jina TANZANIA ndio litumike
kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani
Tanganyika na Zanzibar kwa maana hiyo
jina TANZANIA limezaliwa kutoka majina
manne majina hayo ni
Tanganyika,Zanzibar,Iqbal na Ahmadiyya
Mohammed Iqbal Dar baada ya kupata
jina hilo akalituma jina hilo kwenye kamati
ya kuratibu Shindano
Baada ya Muda mwingi kupita baba yake
na Mohammed Iqbal Dar alipokea Barua
nzito kutoka serikalini ikiwa inasomeka
kama ifuatavyo….
REPRESENTED BY THE
MINISTRY OF
INFORMATION AND TOURISM,TANZANIA
TO
MOHAMED
IQBAL DAR
IN RECOGNATION OF THE
ACHIEVEMENT OF CHOOSING THE NEW
NAME FOR THE
UNITED REPUBLIC
OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR NAMELY
“REPUBLIC
OF TANZANIA”
DURING THE NATIONAL
COMPETITION DAY IN 19 TH NOVEMBER
1964
I A
WAKAL
MINISTER FOR
INFORMATION AND TOURRISM
Barua hiyo pia ilisema..
Utakumbuka kuwa miezi michache iliyopita
ulituandikia kutupa ushauri kuhusu jina
jipya la Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar na wewe pamoja na wananchi
wenzio 16 ulishauri nnchi yetu iitwe
Tanzania.Nafurahi kukuarifu kuwa
mshirikiane ile Zawadi y ash.200
iliyoahidiwa na leo nakuletea check ya
sh.12/50 ikiwa ni hisa yako katika zile
sh.200.Nashukuru sana kwa jitihada ya
kufikiri jina la Jamuhuri yetu
Barua ikasainiwa na Idrisa Abdul Wakil
Waziri wa Habari na utalii kipindi hicho.
Sasa kwa nini Mohamedi Iqbal Dar anadai
yeye kuwa mshindi pekee wakati Barua
ilikuwa inaonyeshakulikuwa na washindi
wengine 15 ambao nao walishinda,Jibu ni
kuwa wakati wa kutolewa kwa Zawadi hizo
hakuna aliyejitokeza zaidi ya Bwana
Mohammed Iqbal Dar na Bwana Yusufal
Pir Mohamed ambaye hata hivyo alikosa
sifa baada ya kushindwa kutoa barua ya
kumpongeza kuwa ameshinda kwa madai
kuwa Barua ameipoteza,hivyo Wizara ya
Habari na Utalii iliamua kumtangaza
bwana Mohammed Iqbal Dar kuwa Mshindi
na kumpatia zawadi yote y
ash.200/:pamoja na Ngao.
Bwana Mohammedi Iqbal Dar anasema
anachosikitika ni kuwa Mchango wake
bado Watanzania hawathamini mchango
wake lakini yeye anaipenda Tanzania na
anajivunia kuwa Mtanzania japo anadhani
dini yake ya Uislamu ndio tatizo hawataki
kutambua mchango wake ila anaamini
kuwa siku moja ukweli utajulikana
Hayo ni maelezo ya Mohammed Iqbal Dar
ambaye kwa sasa anaishi Uingereza kwa
kuwa huko ndiko alipata kazi eneo la
Birmigham b35 6ps UK,Dar –es-Salaam
House,18 TURNHOUSE ROAD,PHONE 44
121-747-9822.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni