3 Apr 2016

MFAHAMU NYATI HUYU MWENYE RANGI NYEUPE AMBAYE ALIONEKANA NGORONGORO TU NA SIO SEHEMU NYINGINE YOYOTE DUNIANI.

Kama ilivyo kawaida kwa wanyama wote aina ya nyati huwa na ngozi yenye rangi nyeusi.Hii ilikua tofauti kabisa katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ambapo mwaka 2013 alionekana aina ya nyati mwenye rangi nyeupe ,rangi ambayo ni tofauti kabisa na nyati wengine wote wanaopatikana ulimwenguni.
Nyati huyu aligunduliwa na maafisa wa polisi wanaofanya kazi katika kituo cha polisi ndani ya hifadhi hiyo ambao walieleza kuwa walimwona nyati huyo majira ya asubui akiwa ameongozana na nyati wengine takribani ishirini.Kwa wakati huo.Ngorongoro ilikua na nyati 350 kwa wakati hule.
Tukio hili la kuonekana kwa aina hii ya nyati katika hifadhi ya ngorongoro linaiongezea ubora mbuga hii kwani duniani kote akuna sehemu ambayo nyati wa aina kama hii amewai kuonekana isipokuwa Ngorongoro.
Pia Miss Tanzania mwaka 2013 alipata nafasi ya kwenda kumuelezea na kumtangaza vyema nyati huyu mweupe katika mashindano ya urembo ya dunia.
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ndio inayoongoza kwa kupokea watalii wengi zaidi nchini,kwa mujibu wa Afisa utalii wa shirika hilo,Asantaeli Melita,zaidi ya watalii 585,000 hutembelea eneo hilo,na hasa kreta kila mwaka.
Tanzania kwa ujumla hupata watalii  milioni moja kwa mwaka.
Mbali ya nyati huyu wa ajabu kugunduliwa Ngorongoro,eneo hili lina maajabu mengine kadhaa,ukiwemo kilima cha mchanga kinachotembea bila kusambaratika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni