8 Apr 2016

HUU NDIO UKOO WA KIMASAI UNAOSEMEKANA KUWA NA UNDUGU NA WANYAMA,UNAITWA 'MOLLEL' UNAPATIKANA NGORONGORO.

Arusha. Licha ya umaarufu wake, Hifadhi ya Taifa Ngorongoro iliyopo mkoani Arusha ina mambo mengi ya kuvutia yanayoifanya muda wote kuwa ya kipekee duniani. 
Upekee huo unatokana na mfumo wa maisha ya binadamu yanavyohusiana moja kwa moja na maisha ya wanyama. 

Siyo jambo geni kusikia kuwa binadamu hasa wa jamii ya Kimasai wanaoishi kwenye eneo la hifadhi hiyo wanaishi na mifugo yao katika maeneo yaliyo na wanyamapori bila kudhuriana. 

Hata hivyo, jambo linaloweza kuwa geni na la ajabu ni baadhi ya koo za Kimasai ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kuelezwa kwamba ?zina udugu? na baadhi ya wanyama. 

Licha ya maelfu ya watalii kutembelea hifadhi hiyo ili kufaidi na kuona wanyama waliosheheni Ngorongoro, kasi ya wageni hao pia ni kubwa kutembelea jamii ya Wamasai inayoishi eneo hilo ili kujua mila na tamaduni zao na namna wanavyoweza kuishi na wanyama. 

Hakika hakuna ubishi kwamba Wamasai wa Ngorongoro na wanyama katika Hifadhi ya Ngorongoro ni marafiki. 

Ukweli huo unakwenda mbali zaidi na kubainisha kuwa hata baadhi ya koo za Kimasai, ?zina udugu? na wanyama kwa kadri ya majina yao. 

Inaelezwa kuwa kuna ukoo wenye ?udugu? na nyoka, mwingine simba hata wanyama wengine. 

Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Vincent Mbilika anaeleza kuwa zipo koo ambazo majina yao yana uhusiano na wanyama hata wadudu. 

Mfano; ukoo wa Mollel unatajwa kuhusiana na faru, Laitayok unahusiana na tembo na mbogo, nyani na tumbili wanahusianishwa na ukoo wa Ilukumai, ambao fisi na nyoka wanaelezwa kuwa na uhusiano na ukoo wa Illtarru-sero. 

Mbilika anaeleza kuwa katika koo iliyo ndugu na nyoka, jamii hiyo ikikuta nyoka ndani ya nyumba yao haipambani naye tofauti na ilivyo kwa jamii nyingine, zinachofanya ni humwekea maziwa kwa kumwagia, naye huyanywa. 

?Baada ya kupewa maziwa, hutoa ndimi zake na kulamba maziwa kisha hutoka ndani ya nyumba bila kudhuru mtu, tena anatokea mlangoni. Hivyo, koo yenye udugu na nyoka hata kama ni mkubwa kiasi gani, ikiwa ameingia ndani ya nyumba, hata kufikia hatua ya kulala kitandani na mtoto mdogo, hauawi,? anasema Mbilika.

Anasisitiza kuwa koo iliyo na udugu na nyoka ni marufuku kuua nyoka. 

?Huu ni utalii wa aina moja ambao unaweza kuwapo sehemu nyingi nchini na hili ni kwa wanyama wote. Ndiyo sababu Wamasai hawali wanyamapori,? anasema. 

Katika juhudi zake kuhakikisha wananchi wanashiriki masuala ya utalii hasa wa mila na utamaduni, mwaka 1988 NCAA ilianzisha mradi unaohusisha utalii huo pamoja na kuanzisha maboma ya Kimasai yanayotumika kwa utalii. 

Kuanzishwa kwa maboma hayo imekuwa ni faraja kwa wenyeji wa Ngorongoro, kwani sasa yanawapatia fedha kutoka kwa watalii ambao hutembelea kujifunza mila mbalimbali na kuchezewa ngoma. 

Maboma saba 
Seneto ni moja ya maboma saba yaliyo katika eneo la NCAA, yote yakiwa ya kitamaduni. 

Katika maboma hayo, kuna nyumba ndogo zisizopungua 24 ambazo mtalii huweza kuingia na kujifunza mambo mbalimbali ya asili ya Kimasai. 

Kiongozi wa Boma la Seneto, Kimati Sabore anasema kupitia maboma hayo, wameweza kuingiza fedha nyingi.   

Anasema kuwa kwa sasa katika boma hilo ambapo watakaa kwa miaka miwili, kuna watu 124 wanaotoka Kata ya Ngorongoro. 

Sabore anasema katika vijiji vitatu vya kata hiyo, wamechukuliwa kina mama wanane kutoka kila kitongoji na morani 18, huku wengine wakialikwa kupeleka huduma mbalimbali kwenye boma na kusaidia kuimba. 

Anasema kuwa wanapata fedha kwa watalii, wanaoingia katika boma hilo kutazama utamaduni na kwa kila gari linaloingia, hulipa Sh20,000. 

?Wakija huku ndani, wanaona tamaduni zetu, watachezewa ngoma na kununua vitu mbalimbali vya kitamaduni kama shanga na mapambo ya asili,? anasema.

Anasema baada ya kukaa katika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni