1 Apr 2016

HUYU NDIYE 'MATILDA' NYOKA MWENYE PEMBE MBILI ANAYEPATIKANA KUSINI MWA TANZANIA TU.


'MATILDA' ni nyoka wa aina ya pekee duniani ambae anapatikana kusini mwa Tanzania tu.
Nyoka huyu aligunduliwa miaka ya 2010 na 2011 kusini mwa Tanzania na baada ya mda mfupi aliidhinishwa rasmi kama aina mpya ya nyoka duniani.
Jina hili 'MATILDA' Lilitokana na mtoto anayeitwa Matilda amabe alikuwa anapenda sana kumtazama nyoka huyu.Mtoto huyu Matilda alikuwa ni mtoto wa mwanasayansi ambae alikuwa Director wa Wildlife conservation society Tanzania,Mr.Tim Davenport ambae ndiye aliyeongoza utafiti wa nyoka huyu.
Nyoka huyu aina ya 'MATILDA'anayo magamba ya rangi ya njano na nyeusi ,macho ya kijani,urefu wa zaidi ya futi mbili na magamba yaliyojitokeza mfano wa pembe.
Eneo halisi analopatikana nyoka huyu alijatajwa kutokana na sababu za kiusalama wa nyoka hawa  na kuepukana na maalamia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni