24 Apr 2016

HII NDIO 'MANTA RESORT' HOTELI YA KITALII ILIYOJENGWA CHINI YA BAHARI ZANZIBAR KISIWANI PEMBA.

Manta Resort” Hotel hii ya kipekee iliyo visiwani Zanzibar yawa gumzo kwenye Vyombo vya Habari vya Kimataifa...

Ina vyumba chini ya maji na Bei ya kulala kwa siku ni $900 single na a$1,500 double..Hoteli imekua gumzo kwenye vyombo vya habari vya kimataifa na ndio hoteli pekee yenye vyumba vya chini ya maji Barani Africa ambapo mtu akiwa chumbani anaweza ona samaki wakipita nje ya dirisha lake.

Hoteli hii yenye vyumba 16 iitwayo The Manta Resort ikiwa designed by Swedish company Genberg Underwater Hotels kwa mujibu wa CNN.
Yani ukiwa umelala chumbani unaona samaki kabisa kupitia madirisha ambapo gharama yake kulala kwa watu wawili ni dola za Kimarekani 1500 ambayo ni zaidi ya milioni mbili za kitanzania na kwa mtu mmoja ni $900 ambayo inagonga kwenye milioni moja na laki nne hivi.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni