23 Apr 2016

HILI NDIO KABURI LA WAPENDANAO WAWILI WALIOZIKWA PAMOJA HUKU WAMEKUMBATIANA KATIKA KABURI MOJA WILAYANI BAGAMOYO.

Wapendano hao baada ya kukutwa wamekufa
kandokandao ya bahari ya hindi huku wakiwa
wamekumbatiana,walizikwa kwenye kaburi
moja huku wakiwa wamekumbatiana hivyo hivyo
na hili ndio kaburi lao.
Walikutwa wamekufa kwenye uvukwe wa bahari
ya hindi eneo la kijiji cha Kaole wilaya ya
Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

WAPENDANAO wawili mke na mume
walkutwa wamekufa huku wamegandana
kwenye bichi ya ufukwe wa bahari ya hindi kijiji
cha Kaole,Walaya ya Bamoyo Mkoa wa Pwani
na kurazimika kuzikwa kwenye kaburi moja
huku wamekumbatia.
Akizungumza na Mtandao huu Bw Boniface
Sangija'2 Pac' alidai kwamba historia inaonyesha
kwamba wana ndoa hao wapendanao
waliokuwa wakiishi kijiji cha Kaole walikutwa
wamekufa huku wamegandana kwenye ufukwe
wa bahari ya hindi walikoenda kustarehe.
" Hili ni kaburi la wapendanao ambao histori
iliyopo kwenye ofisi za makumbusho ya magofu
haya ya kaole zinaonyesha kwamba wapendanao
hao waliamua kwenda bichi kuogelea bahari ya
hindi eneo hili la Kaole baada ya kuogelea
walikumbatiana eneo la nchi kavu ikiwa ni ishara
ya muendelezo wa upendo wao wa
ukweli"alisema mfanyakazi huona kuongeze
kusema kwamba,
"Histori hiyo imedai kwamba ghafla wanandoa
hao walifikwa na kifo cha ghafla wote wawili
huku wamekumbatiana, wazee wa kalne hiyo 13
waliamua kuwazika kwenye kaburi moja huku
wakiwa wamekumbatiana hivyo hivyo"alisema
mfanyakazi huyo wa eneo hilo la kitalii la Kaole
ambaye kazi yake ni kutoa maelekezo kwa
watalii wa ndani na wale wa nje ya nchi.
Leo makala hii inafika tamati kwenye
makumbusho ya histori za dini ya kiislama
yalipo kijiji cha Kaole Wilaya ya Bagamoyo Mkoa
wa Pwani,kesho makala hii itawaleta histori na
makumbusho wa dini ya kikristo ambayo pia
yako kwenye mji huo wa Bagamoyo eneo la
Misheni .

Maoni 1 :