8 Apr 2016

HICHI NDICHO KITUO CHA TEMBO YATIMA KINACHOPATIKANA ARUSHA NCHINI TANZANIA.


Tanzania ilianzisha kituo cha kwanza cha tembo yatima mjini Arusha.
Kituo hicho kinaifadhi watoto wa tembo waliopoteza wazazi wao kutokana na vitendo vya ujangili au sababu nyengine.
Hatua ya serikali ya kuanzisha kituo hicho inakuja baada ya utafiti wa serikali kubaini kuwa Tanzania hupoteza takriban tembo 30 kila siku.
Kituo hicho kinatoa uangalizi kwa tembo wadogo wapatao 40, na watahifadhiwa mpaka watakapokuwa wakubwa na hatimae kurudishwa katika mazingira yao halisia.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na BBC,Aliyekua  waziri wa Utalii wa Tanzania Lazaro Nyalandu alibaini kwamba katika hifadhi ya taifa ya Ruaha pekee, tembo wapatao 12,000 walitoweka katika kipindi cha mwaka mmoja.
Waziri Nyalandu alikiri kwamba kiwango hicho ni kikubwa mno na kwamba kinatia wasiwasi hivyo kuongeza kwamba uchunguzi umefanyika kubaini chanzo cha tatizo hilo.


Mamlaka maalumu ya Umoja wa Mataifa inayojihusisha na wanyama walio hatarini, imesema kwamba takwimu hizo zinaashiria kwamba Tanzania ni kitovu cha ujangili huku pembe za ndovu zikisafirishwa kupitia bandari ya Dar es
Salaam kwenda nchi jirani.
Tangu mwaka 2009, angalau tani 45 za pembe za ndovu zinaaminika kusafirishwa kwa njia za magendo kutoka Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni