26 Apr 2016

HILI NDIO DARAJA LA KIGAMBONI,DARAJA REFU AFRIKA MASHARIKI LILILOPEWA JINA LA BABA WA TAIFA.



Mnamo April 19 ya mwezi huu daraja la kigamboni lilizinduliwa rasmi na kuanza kutumika kama ilivyopangwa.Mgeni rasmi katika shughuli izo za uzinduzi wa daraja hili alikuwa mheshimiwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu John Pombe Magufuli.
Daraja hili la kisasa linalotajwa kuwa ndio daraja refu kuliko yote Afrika mashariki lina urefu wa mita 680 na upana wa mita 27.5.Daraja hili lina barabara sita za magari na barabara moja ya waenda kwa miguu kila upande.
Daraja hili limepewa jina la baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere licha ya watanzania wengi kupendekeza jina la raisi wa sasa mheshimiwa John Pombe Magufuli Lakini mheshimiwa raisi ye mwenyewe akapendekeza jina la mwalimu Nyerere litumike kama jina la daraja hilo.
Asilimia 60 ya ujenzi wa daraja hili imedhaminiwa na mfuko wa hifadhi ya taifa NSSF na asipimia 40 imetolewa na serikali ya jamhuri ya muungano wa  Tanzania.Daraja hili adi kukamilika limegharimu zaidi ya dola za kimarekani 140.





Muonekano wa daraja hill wakari wa usiku.

24 Apr 2016

LIFAHAMU KWA KINA JIWE HILI KUBWA MWANZA,LINAUKUBWA WA HEKARI ZAIDI YA MBILI NA LINAMKUSANYIKO WA MAWE TAKRIBANI ELFU NNE(4000) JUU YAKE.

Source;GSENGO.BLOGSPOT.COM

Njia kuelekea Jiwe Kuu inachangamoto zake ni barabara inayopitika kimtindo.
Taswira kuelekea Jiwe Kuu Kitangiri Mwanza.
Rock City.
Kutoka moja ya vilele vya Jiwe kuu utakuwa na fursa ya kuona maadhari ya Malaika Beach Resort Mwanza.
Team Yangu ya Utalii ikiwa na wadau Bodi ya Utalii Tanzania..
Moja kati ya mawe ya heshima.
Mabango.
Team #iLoveMwanza #JembekaFestival2016 #Jembeka NaVodacom
Bob White katika moja ya angle za Jiwe Kuu ambako kuna mawe ya historia.
Gsengo at the area.
Vijito juu ya jiwe Kuu.
Kileleni Jiwe Kuu.
Juu kabisa Jump Jump zinahusika....
Wow...
safiii......
The view from the top...!!
Hapa ndipo mahala mmoja wa watemi wa Kabila la wasukuma mwenye historia kubwa Mwanamalundi aliketi panaitwa Matako ya Mwanamalundi.
Jiwe Kuu hili ni jiwe moja lenye ukubwa wa kama hekari mbili hivi ambapo juu yake kuna mawe zaidi ya 4000 yaliyojikita sehemu na sehemu kuleta mvuto wa kipekee katika muonekano.
Kutokana na utulivu unaotawala eneo hili na upekee wa mawimbi ya sauti ukimya umesababisha wahubiri na watumishi wa makanisa kulitumia eneo hili kama sehemu ya ibada.
Kona katikati ya mawe upenuni.
Mungu kweli ameumba dunia Jiwe hili ni kama limejiegesha lakini jinsi lilivyojishikiza ni kwaaina ya kipekee kama limejishikiza hivi,, ukadhani linaweza kuanguka lakini kumbe ahata usukume vipi halianguki,
Let us try.....aaaaah wapi.!!!
Blogger Gsengo at the place
Getto juu ya mwamba.
Mnyama huyu anaitwa pimbi akimbii hats akirushiwa jiwe.

HII NDIO 'MANTA RESORT' HOTELI YA KITALII ILIYOJENGWA CHINI YA BAHARI ZANZIBAR KISIWANI PEMBA.

Manta Resort” Hotel hii ya kipekee iliyo visiwani Zanzibar yawa gumzo kwenye Vyombo vya Habari vya Kimataifa...

Ina vyumba chini ya maji na Bei ya kulala kwa siku ni $900 single na a$1,500 double..Hoteli imekua gumzo kwenye vyombo vya habari vya kimataifa na ndio hoteli pekee yenye vyumba vya chini ya maji Barani Africa ambapo mtu akiwa chumbani anaweza ona samaki wakipita nje ya dirisha lake.

Hoteli hii yenye vyumba 16 iitwayo The Manta Resort ikiwa designed by Swedish company Genberg Underwater Hotels kwa mujibu wa CNN.
Yani ukiwa umelala chumbani unaona samaki kabisa kupitia madirisha ambapo gharama yake kulala kwa watu wawili ni dola za Kimarekani 1500 ambayo ni zaidi ya milioni mbili za kitanzania na kwa mtu mmoja ni $900 ambayo inagonga kwenye milioni moja na laki nne hivi.




23 Apr 2016

HICHI NDICHO KITUO CHA REDIO NA TV KITAKACHOIPA HESHIMA LUGHA YA 'KISWAHILII' KWA KUTUMIA LUGHA HII KAMA JINA LA KITUO HICHO.

Afrika Swahili media ni kituo cha Redio na Tv Kinachoipa heshima lugha ya Kiswahili kwa kutumia lugha hio kama jina halisi la kituo hicho yani yani 'SWAILI FM' Na 'SWAHILI TV'.
Kituo hicho kinatarajiwa kufunguliwa ndani ya wiki mbili zijazo nchini hapa ambapo studio za Redio hii zitakua mkoani Morogoro na za TV zitakua Dar Es Salaam.
Kituo hichi kimejizatiti kuajiri vijana wengi wa kitanzania wenye taranta na vipaji mbalimbali kwenye Sanaa hususa Utangazaji.
Frequency za redio hio ni 93.1 Morogoro.

TAZAMA MAKTABA YA SHULE YA MSINGI ALIYOSOMA MWALIMU NYERERE,NI SHULE YA MSINGI MWISENGE

Samani zilizomo ndani ya maktaba hiyo kabla ya kuwekwa vitabu.Maktaba hiyo imejengwa na kuwekwa samani pamoja na vitabu na shirika la HakiElimu ikiwa ni njia mojawapo ya kumuenzi baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere.

Muonekano wa pembeni ndani ya maktaba ya Shule ya Msingi Mwisenge.Mwl Nyerere alisoma shule hii.


Maktaba inavyoonekana kwa nje


Nukuu ya maneno ya Mwalimu Nyerere kuhusu elimu ikiwa ndani ya maktaba

HILI NDIO KABURI LA WAPENDANAO WAWILI WALIOZIKWA PAMOJA HUKU WAMEKUMBATIANA KATIKA KABURI MOJA WILAYANI BAGAMOYO.

Wapendano hao baada ya kukutwa wamekufa
kandokandao ya bahari ya hindi huku wakiwa
wamekumbatiana,walizikwa kwenye kaburi
moja huku wakiwa wamekumbatiana hivyo hivyo
na hili ndio kaburi lao.
Walikutwa wamekufa kwenye uvukwe wa bahari
ya hindi eneo la kijiji cha Kaole wilaya ya
Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

WAPENDANAO wawili mke na mume
walkutwa wamekufa huku wamegandana
kwenye bichi ya ufukwe wa bahari ya hindi kijiji
cha Kaole,Walaya ya Bamoyo Mkoa wa Pwani
na kurazimika kuzikwa kwenye kaburi moja
huku wamekumbatia.
Akizungumza na Mtandao huu Bw Boniface
Sangija'2 Pac' alidai kwamba historia inaonyesha
kwamba wana ndoa hao wapendanao
waliokuwa wakiishi kijiji cha Kaole walikutwa
wamekufa huku wamegandana kwenye ufukwe
wa bahari ya hindi walikoenda kustarehe.
" Hili ni kaburi la wapendanao ambao histori
iliyopo kwenye ofisi za makumbusho ya magofu
haya ya kaole zinaonyesha kwamba wapendanao
hao waliamua kwenda bichi kuogelea bahari ya
hindi eneo hili la Kaole baada ya kuogelea
walikumbatiana eneo la nchi kavu ikiwa ni ishara
ya muendelezo wa upendo wao wa
ukweli"alisema mfanyakazi huona kuongeze
kusema kwamba,
"Histori hiyo imedai kwamba ghafla wanandoa
hao walifikwa na kifo cha ghafla wote wawili
huku wamekumbatiana, wazee wa kalne hiyo 13
waliamua kuwazika kwenye kaburi moja huku
wakiwa wamekumbatiana hivyo hivyo"alisema
mfanyakazi huyo wa eneo hilo la kitalii la Kaole
ambaye kazi yake ni kutoa maelekezo kwa
watalii wa ndani na wale wa nje ya nchi.
Leo makala hii inafika tamati kwenye
makumbusho ya histori za dini ya kiislama
yalipo kijiji cha Kaole Wilaya ya Bagamoyo Mkoa
wa Pwani,kesho makala hii itawaleta histori na
makumbusho wa dini ya kikristo ambayo pia
yako kwenye mji huo wa Bagamoyo eneo la
Misheni .

8 Apr 2016

HICHI NDICHO KITUO CHA TEMBO YATIMA KINACHOPATIKANA ARUSHA NCHINI TANZANIA.


Tanzania ilianzisha kituo cha kwanza cha tembo yatima mjini Arusha.
Kituo hicho kinaifadhi watoto wa tembo waliopoteza wazazi wao kutokana na vitendo vya ujangili au sababu nyengine.
Hatua ya serikali ya kuanzisha kituo hicho inakuja baada ya utafiti wa serikali kubaini kuwa Tanzania hupoteza takriban tembo 30 kila siku.
Kituo hicho kinatoa uangalizi kwa tembo wadogo wapatao 40, na watahifadhiwa mpaka watakapokuwa wakubwa na hatimae kurudishwa katika mazingira yao halisia.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na BBC,Aliyekua  waziri wa Utalii wa Tanzania Lazaro Nyalandu alibaini kwamba katika hifadhi ya taifa ya Ruaha pekee, tembo wapatao 12,000 walitoweka katika kipindi cha mwaka mmoja.
Waziri Nyalandu alikiri kwamba kiwango hicho ni kikubwa mno na kwamba kinatia wasiwasi hivyo kuongeza kwamba uchunguzi umefanyika kubaini chanzo cha tatizo hilo.


Mamlaka maalumu ya Umoja wa Mataifa inayojihusisha na wanyama walio hatarini, imesema kwamba takwimu hizo zinaashiria kwamba Tanzania ni kitovu cha ujangili huku pembe za ndovu zikisafirishwa kupitia bandari ya Dar es
Salaam kwenda nchi jirani.
Tangu mwaka 2009, angalau tani 45 za pembe za ndovu zinaaminika kusafirishwa kwa njia za magendo kutoka Tanzania.