Hii orodha ya makabila ya Tanzania inaweza kuwa na matatizo kwenye majina kadhaa, kwa sababu mbalimbali.
Orodha hii inatokana na orodha ya lugha za Tanzania inayopatikana katika Ethnologue, pamoja na tovuti nyingine.
Inawezekana kwamba baadhi ya majina ya makabila ni majina ya lugha au lahaja tu, badala ya makabila, na labda majina mengine yaliandikwa vibaya.
Juu ya hiyo, hakuna ufafanuzi wa wazi kusema kikundi fulani ni kabila au siyo. Vikundi kadhaa katika orodha hii vina wenyeji mamia tu, lakini vikundi vingine vina mamilioni ya watu; labda kila kikundi kinaitwa "kabila," lakini ni jamii za aina tofauti kabisa. Vikundi katika ukurasa huu vimeorodheshwa kuwa vikundi tofauti kutokana na ushahidi kutoka Ethnologue kutofautisha lugha zao.
Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani.
Orodha hii haizingatii makabila yanayoishi katika Tanzania kama wakimbizi tu, hasa kutokana na vita katika nchi za jirani. Vilevile ukurasa huu hauorodheshi vikundi vya wahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Uarabuni au Uhindi.
- Waalagwa (pia wanaitwa Wasi)
- Waakiek
- Waarusha
- Waassa
- Wabarabaig (pia wanaitwa Wamang'ati)
- Wabembe
- Wabena
- Wabende
- Wabondei
- Wabungu (au Wawungu)
- Waburunge
- Wachagga
- Wadatoga
- Wadhaiso
- Wadigo
- Wadoe
- Wafipa
- Wagogo
- Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome)
- Wagweno
- Waha
- Wahadzabe (pia wanaitwa Wahadza na Watindiga)
- Wahangaza
- Wahaya
- Wahehe
- Waikizu
- Waikoma
- Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu)
- Waisanzu
- Wajiji
- Wajita
- Wakabwa
- Wakaguru
- Wakahe
- Wakami
- Wakara (pia wanaitwa Waregi)
- Wakerewe
- Wakimbu
- Wakinga
- Wakisankasa
- Wakisi
- Wakonongo
- Wakuria
- Wakutu
- Wakw'adza
- Wakwavi
- Wakwaya
- Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele)
- Wakwifa
- Walambya
- Waluguru
- Waluo
- Wamaasai
- Wamachinga
- Wamagoma
- Wamakonde
- Wamakua (au Wamakhuwa)
- Wamakwe (pia wanaitwa Wamaraba)
- Wamalila
- Wamambwe
- Wamanda
- Wamatengo
- Wamatumbi
- Wamaviha
- Wambugwe
- Wambunga
- Wamosiro
- Wampoto
- Wamwanga
- Wamwera
- Wandali
- Wandamba
- Wandendeule
- Wandengereko
- Wandonde
- Wangasa
- Wangindo
- Wangoni
- Wangulu
- Wangurimi (au Wangoreme)
- Wanilamba (au Wanyiramba)
- Wanindi
- Wanyakyusa
- Wanyambo
- Wanyamwanga
- Wanyamwezi
- Wanyanyembe
- Wanyaturu (pia wanaitwa Warimi)
- Wanyiha
- Wapangwa
- Wapare (pia wanaitwa Wasu)
- Wapimbwe
- Wapogolo
- Warangi (au Walangi)
- Warufiji
- Warungi
- Warungu (au Walungu)
- Warungwa
- Warwa
- Wasafwa
- Wasagara
- Wasandawe
- Wasangu (Tanzania)
- Wasegeju
- Washambaa
- Washubi
- Wasizaki
- Wasuba
- Wasukuma
- Wasumbwa
- Waswahili
- Watemi (pia wanaitwa Wasonjo)
- Watongwe
- Watumbuka
- Wavidunda
- Wavinza
- Wawanda
- Wawanji
- Waware (inaaminika lugha yao imekufa)
- Wayao
- Wazanaki
- Wazaramo
- Wazigula
- Wazinza
- Wazyoba
Dah!!nashukuru sana kwa orodha hii,nimeipenda sanaaa💝💘
JibuFutaSio wapogolo ni wapogoro
JibuFuta