Bongo Ride Na Team Tezza ni makundi ya vijana wa kitanzania yanayojihusisha na sanaa na burudani za uendeshaji wa magari.Vijana hawa ufanya sanaa za magari kwa lengo la kuibua na kuonesha matatizo yanayoikumba jamii pasipo jamii kuwa na uelewa mkubwa wa matatizo hayo.Vijana hawa wamekuwa wakifanya sanaa hizi kwa nyakati mbalimbali huku wakionesha matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii.
Mwaka huu vijana hawa wa Bongo Ride Na Team Tezza wamekua wakipinga na kupiga vita mauaji dhidi ya wanyama pori ,tatizo ambalo limeonekana kushamiri sana nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.Kauli mbiu yao katika kupinga janga hili ni 'YOUTH AGAINST POACHING' yani 'VIJANA DHIDI YA UJANGILI WA WANYAMAPORI'
Ni tatizo linaloshika kasi siku baada ya siku na linatishia amani katika sekta ya utalii kwani kuna hatihati ya wanyama pori hususa ni tembo kupungua kwa idadi kubwa au kwisha kabisa katika mbuga zetu za wanyama kitu ambacho kitapunguza idadi ya watalii wanaokuja Tanzania kwa ajili ya kuwaona tembo.
Vijana hawa wameamua kutilia mkazo swala hili na kupinga vikali mauaji haya dhidi ya wanyamapori kupitia sanaa zao za magari.
Tarehe 25 Ya mwezi huu vijana hawa walisafiri kuelekea Arusha katika mbuga ya TARANGILE NATIONAL PARK kwa ajili ya kujifunza vitu mbalimbali kuhusu wanyama pori na kusistiza jamii juu ya shuguli za utalii wa ndani ya nchi [Domestick Tourism].
Safari hii ilikua na lengo kubwa la vijana hawa kuwahamasisha vijana wenzao kushiriki vita hii kali dhidi ya mauaji ya wanyama pori kwa kuungana nao katika safari hii ili wote wapate kujua umuhimu wa kuwa na wanyama hawa na madhara ya kuua wanyama hawa kitu ambacho kinaongeza uelewa juu ya jinsi ya kupambana na janga hili.
Wamekaa Arusha kwa muda wa siku tatu na safari yao ya kutoka Dar es salaam adi Arusha iliambatana na sanaa zao za magari yaliyokua yameongozana kwa msafara mmoja.
Pichani ni picha zinazowaonesha viongozi wa makundi haya yavijana wakifanyiwa mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari kabla ya safari hayo ya kuelekea huko mbugani TARANGIRE,ARUSHA.
Picha zinazofuta ni matukio mbalimbali ya vijana hao wakiwa safarini kuelekea TARANGIRE mpaka wanafika mbugani huko;
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni