31 Mac 2016

HUYU NDIYE TWIGA MWENYE ULEMAVU WA NGOZI[ALBINO /KISAYANSI ANAITWA 'OMO'] ANAYEPATIKANA TANZANIA ,MKOANI ARUSHA KATIKA MBUGA YA TARANGILE.

Twiga huyu mwenye ulemavu wa ngozi ambae kisayansi anajulikana kwa jina la 'OMO' aligunduliwa na Dk.Derek Lee katika mbuga ya TARANGIRE,Mkoani Arusha  wakati dokta huyo akifanya  uchunguzi na utafiti wa wanyama mbalimbali.
Dk.Lee alimgundua twiga huyu mwenye ulemavu wa ngozi kutokana na utofauti wake na twiga  wenzake ambao wanapatikana katika mbuga hiyo.Twiga huyu alioneakana akiongozana na twiga  wenzake sehemu mbalimbali za mbuga hiyo bila ya twiga wenzake kumshangaa wala kumtenga twiga huyu Albino.
 Mnyama huyu ni mnyama  alietofauti sana na wanyama wenzake katika kipengele cha rangi kwani rangi yake ni ile nyeupe ya kukolea inayofanana kabisa na rangi ya binadamu mwenye ulemavu wa ngozi.
Gazeti moja la kimarekani lilitoa ripoti kwamba twiga wa aina hii yani mwenye ulemavu wa ngozi ni wachache sana hapa duniani na kama twiga huyu atatunzwa vizuri basi atakuja kuwa moja ya kivutio kikubwa sana cha utalii hapa duniani.
Licha ya kutokutengwa na twiga wenzake lakini twiga huyu yuko katika hatihati ya kuhuliwa na wanyama wenzake tofauti na swala kutokana na muonekano wa tofauti na wenzake kitu ambacho kina watisha baadhi ya wanyama wenzake.
DK.Leek alisema twiga huyu anatakiwa kupewa ulinzi wa kutosha ili kumzuia kujeruhiwa vikali au kuhuliwa kabisa na wanyama wenzake.Pia DK.Leek alisema mnyama huyu yuko katika hatihati ya kuuliwa na baadhi ya binadamu kutokana na mwonekano unaoweza kuwafanya baadhi ya binadamu kutamani kujua radha aliyonayo mnyama huyu endapo ataliwa kama chakula.


Pichani ni twiga huyu albino 'OMO' akiwa mbugani TARANGILE ,mkoani Arusha.



KUTANA NA BONGO RIDE NA TEAM TEZZA, VIJANA WAKITANZANIA WANAOPINGA UJANGIRI WA WANYAMA PORI KUPITIA SANAA.


Bongo Ride Na Team Tezza ni makundi ya vijana wa kitanzania yanayojihusisha na sanaa na burudani za uendeshaji wa magari.Vijana hawa ufanya sanaa za magari kwa lengo la kuibua na kuonesha matatizo yanayoikumba jamii pasipo jamii kuwa na uelewa mkubwa wa matatizo hayo.Vijana hawa wamekuwa wakifanya sanaa hizi kwa nyakati mbalimbali huku wakionesha matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii.

Mwaka huu vijana hawa wa Bongo Ride Na Team Tezza wamekua wakipinga na kupiga vita mauaji dhidi ya wanyama pori ,tatizo ambalo limeonekana kushamiri sana nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.Kauli mbiu yao katika kupinga janga hili ni 'YOUTH AGAINST POACHING' yani 'VIJANA DHIDI YA UJANGILI WA WANYAMAPORI'
Ni tatizo linaloshika kasi siku baada ya siku na linatishia amani katika sekta ya utalii kwani kuna hatihati ya wanyama pori hususa ni tembo kupungua kwa idadi kubwa au kwisha kabisa katika mbuga zetu za wanyama kitu ambacho kitapunguza idadi ya watalii wanaokuja Tanzania kwa ajili ya kuwaona tembo.
Vijana hawa wameamua kutilia mkazo swala hili na kupinga vikali mauaji haya dhidi ya wanyamapori kupitia sanaa zao za magari.

Tarehe 25 Ya mwezi huu vijana hawa walisafiri kuelekea Arusha katika mbuga ya TARANGILE NATIONAL PARK kwa ajili ya kujifunza vitu mbalimbali kuhusu wanyama pori na kusistiza jamii juu ya shuguli za utalii wa ndani ya nchi [Domestick Tourism].
Safari hii ilikua na lengo kubwa la vijana hawa kuwahamasisha vijana wenzao kushiriki vita hii kali dhidi ya mauaji ya wanyama pori kwa kuungana nao katika safari hii ili wote wapate kujua umuhimu wa kuwa na wanyama hawa na madhara ya kuua wanyama hawa kitu ambacho kinaongeza uelewa juu ya jinsi ya kupambana na janga hili.
Wamekaa Arusha kwa muda wa siku tatu na safari yao ya kutoka Dar es salaam adi Arusha iliambatana na sanaa zao za magari yaliyokua yameongozana kwa msafara mmoja.

Pichani ni picha zinazowaonesha viongozi wa makundi haya yavijana wakifanyiwa mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari kabla ya safari hayo ya kuelekea huko mbugani TARANGIRE,ARUSHA.


 Picha zinazofuta ni matukio mbalimbali ya vijana hao wakiwa safarini kuelekea TARANGIRE mpaka wanafika mbugani huko;