19 Jul 2016

ITAZAME SARAFU YA SHILINGI ELFU HAMSINI(50) YA KITANZANIA.

Pichani ni sarafu  yenye thamani ya shilingi elfu hamsini za kitanzania iliyozinduliwa siku ya mapinduzi mwaka huu.
Sarafu hii imetengenezwa 92% na madini ya fedha.

ZIFAHAMU FURSA KUMI(10) ZA MAFANIKIO TANZANIA.


Miezi michache iliyopita Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahaba Alizitaja fursa kumi za mafanikio hapa nchini Tanzania baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu.
Ruge Mutahaba alizitaja fursa izo ambazo kila mtu anaweza akazitumia  kwani zinaanzia na mtaji wa kawaida sana wa laki tano(5).
Fursa Namba 1: Biashara kwenye sekta ya Kilimo (Agri business) . Kilimo ndio msingi wa kila kitu, Watanzania wengi wanalima ili wapate chakula ila si kwa ajili ya biashara. Jambo hili linatoa nafasi kwa watu kuweza kuwekeza kwani kupitia Kilimo tutakuwa na viwanda na watu wengi wataweza kujiajiri.
Fursa namba 2: Biashara ya Chakula (Food Business). Fursa hii naitazama kwenye kuongeza dhamani katika biashara na kuzidiwa kujitangaza, usipike tu kwa kawaida, ila ifanye kwa utofauti ikue na kuongeza kipato.
Fursa Namba 3: Biashara katika sekta ya Mauzo, Manunuzi ya rejareja na Usambazaji kupitia njia ya mtandao (Retail – E commerce). Unaweza kutumia mitandao kuuza bidhaa zako na kununua pia. Sio lazima ukutane na mteja ana kwa ana ila kupitia mtandao unaweza kuanza nguo, viatu na vitu vingine.
Fursa namba 4: Biashara katika tasnia ya Habari na Burudani(Media&Entertaiment . Tukiweza kutengeneza film bora zitasaidia kufikisha tasnia hii mbali. Nigeria wamerekodi filamu moja Marekani, ndani ya mwezi mmoja imeuza kopi laki 5. Na wakati wa sisi kuwekeza zaidi na zaidi ili tufikie huko.
Fursa namba 5: Biashara kwenye sekta ya Huduma za Kijamii. Kwa sasa Tunaona Hospitali na Shule nyingi za binafsi na zinafanya vizuri sana. Hi ni nafasi kwetu kuwekeza.
Fursa Namba 6 : Biashara katika Tasnia ya Mitindo na Urembo (Beuty &Fashion). zamani wote kwa mtazamo wetu mwonekano, mvuto ulitokana na fahari ya mtu mwenyewe alichozaliwa nacho, lakini katika ulimwengu wa sasa mwonekano wa mtu ni ‘featuring’ ya vitu vingi sana kuanzia nywele, kucha, make up, fursa zipo nyingi mf. Sasa hivi unaweza kuambiwa kufanya ‘pedicure & manicure’ ni shs elfu 40 hicho ni kimoja tu”Ruge Mutahaba
Fursa Namba 7: Biashara ya Mashamba, Majengo/Mali isiyohamishika (Real Estate) . Tunaona Shule zinaongezeka na Vyuo pia. Hii inatoa nafasi kwa Watanzania kuwekeza kwa kujenga Hostel ambazo zitatoa huduma kwa Wanafunzi na ni kitu cha kudumu.
Fursa namba 8: Biashara katika sekta ya Usambazaji na Usafirishaji (Transport and Logistics).
Fursa namba 9: Sekta ya huduma za kifedha (Financial services) mfano ununuzi wa hisa. “Uelewa kuhusu masuala ya Hisa umekua sana na hii ni fursa nzuri sana kwa Vijana kama wataanza sasa kuwekeza katika Hisa”.
Fursa namba 10: Intaneti na Teknolojia . Mambo mengi sana kwa sasa yanafanyika kupitia mitandao. Watu wanaweza kufanya biashara kupitia mitandao Hii ni nafasi kwetu sisi kuweza kuwekeza. Hii itatupa nafasi ya kujiajiri na pia kwenda na wakati.